Saturday 19 May 2007

Kitchen

Hapa ugomvi sitaki mkaa nje.....! na jiko lako la mkaa jenga kibanda nje, hata kwenye coridor NO! moshi utaingia,
Rangi hii inahitaji usafi, baada ya shudhuli zako jikoni unasafisha na kupanga vizuri na ka-ua pembeni safi, hata mgeni akija nyumbani kwako hajiulizi mara mbili kama akikaribishwa kula. Kunan yumba nyingine loh! unatamani kukimbia ukiambiwa karibu kula, pia kwa wenzangu akina dada, jikoni ndio kioo chako, kunaeleza bayana jinsi ulivyo. Kitaalamu tunasema sebuleni ni usoni na jikoni ni mwilini, kama wewe ni muosha uso tu basi tutajua tukiingia jikoni. kale katabia ka kusafisha sebuleni tu na kuacha sehemu nyingine za nyumba (LOL)

1 comment:

Anonymous said...

nimepapenda hapo jamani. panapendeza sana