Tuesday 25 September 2012

Mwanga ndani ya nyumba

Mwanga ndani ya nyumba ni kitu muhimu sana. Mara nyingi kwa nyumba zetu tulizozozea tuna taa moja tu kubwa juu kwenye dari. Ni kweli inaleta mwanga lakini kwa sisi wapenda mapambo mwanga mzuri na wa aina tofauti ni muhimu sana katika kupendezesha nyumba yako.

picha hii inaonyesha jinsi jikoni kunavyotakiwa kuwa na mwanga mzuri, ukiangalia vizuri utaona madirisha ni makubwa na yenye kupitisha mwanga vizuri lakini pia mpambaji ameongeza pia kwa kuweka nakshi za taa zaidi ya moja ili hata usiku mwanga uwe wa kutosha. katika picha hii utaona pia shades za blue hapo juu, kwenye post yangu itakayofuata nitaongelea kuhusu lamp shades.