Tuesday 25 September 2012

Jinsi ya kupima shades

Wakati wa kununua lamp shade mpya, utakutana na shades za kila namna na kila rangi na kila saizi.ila vipimo hivi nitakavyokuonyesha hapa ni vile utavikuta kila mahali ulimwenguni. Hakikisha una rula, kalamu na karatasi wakati wa kununua shades zako ili usije nunua usiyi ihitaji (lol)





Hivi ni vipimo vinne unavyovihitaji kwa ajili ya ununuzi wa shades zako:
A – Upana/mzunguko  wa juu
B – Upana/mzunguko wa chini.
C – Urefu wa pembeni .
D – Urefu wa katikati.  Kama ionekanavyo kwenye picha hapo juu.
Zaidi ya hiyo utatakiwa kujua, aina ya viungio vilivyo ndani ya shade zako na aina ya bulb utakayotumia.